BURUDANI/UDAKU

CHEK WADADA WALIVYOPAGAWA SHOO 
  YA 
OMMY DIMPOZ







 DIVA KWENU SISI KWETU MRUPO TUU
hii imejionyesha wazi pale mkali wa kenya alivyo badili demu,toa kitu weka kitu.....
sasahivi mkali huyu yuko na kifaa cha kichaga kinachoenda kwa jina la Stallisha Tilya,
hope full utakua ume sema sawaaaaaaaaa!


 

 

 

RAY C ANENEPA GHAFLA, MASHABIKI WA BONGO FLEVA WAMSHANGAA..!! 


Mwanamuziki staa wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ambaye amepotea katika anga la muziki kwa kipindi kirefu kutokana na matatizo ya matumizi ya madawa ya kulevya, amejitokeza akiwa amefutuka. Hivi karibuni, Ray C ameibuka na kuanza kutundika picha na vipande vya video zake katika kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii, ikiwa ni sehemu ya kujiweka karibu na mashabiki wake.
Kufuatia ishu hiyo, kumeibuka mshtuko mkubwa kwa baadhi ya watu kutokana na picha hizo kumuonesha ‘bidada’ akiwa amenenepeana ghafla tofauti na alivyozoeleka
.
 
UNENE UNATOKANA NA DOZI?
Baadhi ya mashabiki wake katika mtandao wa Instagram walidai kuwa inawezekana unene huo unatokana na dozi ya kuacha ‘unga’.
Hata hivyo, wengine walimshukuru Mungu kwa kuwa sasa afya ya mwanadada huyo inaonekana kurudi katika hali yake ya kawaida tofauti na miezi kadhaa aliporipotiwa na gazeti hili akiwa amezimika kutokana na matumizi ya unga.

ABONGEKA
Katika picha hizo, Ray C anaonekana kufutuka usoni, kifuani na mapajani ambapo awali kabla ya matatizo hakuwa hivyo.
Wengi walimshukuru Mungu kumuona tena Ray C akiwa mzima pamoja na ukimya wake katika muziki.
Ray C amekuwa akitundika picha hizo kwa ajili ya mashabiki na marafiki hasa kupitia Instagram akiambatanisha na maelezo huku nyingine zikizungumza zenyewe.

HATAKI KUTAJA ANAPOISHI
Maelezo ya picha hizo yamekuwa yakielezea maisha ya Ray C kwa sasa akiwa kwenye mjengo wa maana bila kutaja ni sehemu gani.
Kwa mujibu wa mashabiki wa Ray C, mwanadada huyo kwa sasa anakula bata tu huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anamuita ‘Daddy’ kwa kuwa ndiye aliyemsaidia kimatibabu.

DAKTARI ANASEMAJE?
Daktari mmoja maarufu jijini Dar aliyehojiwa na gazeti hili, alibainisha kuwa kinachosemwa na mashabiki wa Ray C kwamba kinachomnenepesha ni dozi ya kuacha madawa ya kulevya, kinaweza kuwa kweli au kisiwe kweli.
Aliongeza kuwa kunenepa kunachangiwa na vitu vingi kama kupata maisha mazuri yasiyohusisha msongo wa mawazo au mihangaiko ya hapa na pale hivyo anachofanya ni kula, kulala na kustarehe tu.

 

 

 

 

Arsenal yamwambia RVP: 'huendi popote'       



KWA mujibu wa mtandaoo wa Goal.com, Arsenal inajiandaa kumwambia mshambulaiji wa timu hiyo Robin Van Persie kuwa hataruhusiwa kuondoka katika usajili unaoendelea sasa.

Inaaminika kuwa mshambulaiji huyo raia wa Uholanzi atashikilia msimamo wake wa kutaka kuhama Arsenal wakati atakapokutana tena na Arsene Wenger pamoja na mtendaji mkuu Ivan Gazidis kwa ajili ya mazungumzo upya.

Lakini baadhi ya maofisa wa Arsenal wametonya kuwa klabu hiyo iko tayari kumpoteza bure mchezaji huyo kuliko kumwacha aondoke sahivi.

Hatua hiyo ya Arsenal kumng'ang'ania Van Persie inaonekana na watu wengi ni kama vile kumkomoa mshambuliaji huyo.

Arsenal wanajua kuwa Van Persie atafikisha miaka 30 ifikapo oktaba 2013 na amekuwa akikabiliwa na majeruhi mara kwa mara. Hivyo Arsenal wanaona kuwa huenda timu ambazo zinamvizia sahivi zisimvizie tena mwakani.

"Hatutamruhusu Van Persie kuondoka na tutahakikisha kuwa anamalizia mkataba wake. Atakapofikisha miaka 30, hakuna timu ambayo itakuwa tayari kumlipa mshahara mkubwa. Hivyo itakuwa rahisi kusaini mkataba mpya." Kilisema chanzo kimoja cha karibu na Arsenal.

Arsenal inatarajiwa kusafiri na Van Persie siku ya Jumamosi kwenda Kuala Lumpur, Malaysia kucheza mechi tatu za kiarafiki ambapo moja kati ya mechi hizo itakuwa dhidi ya Manchester City.
AddThis Social Bookmark Button


No comments:

Post a Comment