UTABIRI WA MWAKA 2013 TOKA KWA HASSAN YAHYA HUSSEIN
Mwaka wa 2013 umeanzia siku yaJumanne, siku hii inatawaliwa
Na Sayari ya Mars au Mariikh ambayo
nyota zake ni mbili nazo ni nyota ya Punda au Aries na Nge ambayo
ni Kinyota hii nyota ya Punda ni nyota ya mwanzo ambayo ndio kichwa na
kama nyumba ya Mwanzo na maana yake ni Mwanzo wa jambo, Anza jambo,Tangaza jambo au kupata mafanikio.
Nyota
ya Pili ni NGE au Scorpio ambayo Kinyota ni nyota ya Nane au Nyumba ya
Nane, nyota hi iinaashiria, Hasira, kupotea, Kuachana, kukimbiwa,
Maziko,Vifo na Wasiwasi
Kwa
kawaida Mwaka ukianzia siku ya Jumanne unaashiria Matatizo makubwa,
ikiwa ni pamoja na kuongezeka Vita sehemu mbali mbali za dunia,
Viongozi wa kidini, kisiasa, na kijamii kuugua sana na wengine kufa,
kutokea moto katika miji mikubwa, ukame, ukosefu wa Maadili, wafanyakazi
kuwapiga mabosi wao, uongo kuwa mwingi kwa maana propaganda, umbeya,
masengenyo, mashujaa kufariki, mazao kupungua, ajali kuwa nyingi za bara
na baharini na angani, watu kuwa na khofu na watu wengi kuuwawa
Kwa upande mwingine inaashiria biashara kuongezeka na neema kuwa kubwa na watu kufaidika katika biashara
Pamoja
na hayo kutakuwa na Matatizo ya maradhi kwa watoto hasa kuugua vifua na
maradhi ya kichwa, wanawake wajawazito kupoteza maisha kwa wingi au
kuzaa kwa matatizo makubwa
Kwa
upande wa Siasa Mwaka ukianzia siku ya Jumanne basi hutokea kwamba
Viongozi wa Kidini na kisiasa kutoa matamshi ya utatanishi na
kusababisha khofu kubwa na hata watu kupigana lakini hali hiyo hudumu
kwa muda mfupi, baadhi ya viongozi hukaa pamoja na kukubaliana mambo
baina yao na kurejesha hali ya utulivu na amani
Mwaka
huu wa 2013 Mwezi utapatwa mara tatu tarehe 25/4/2013 ambayo itakuwa
siku ya Alkhamisi, tarehe 25/5/2013 ambayo itakuwa siku ya Jumapili na
tarehe 18/10/2013 siku ya Ijumaa
Jua
lenyewe nalo lipatwa mara mbili tarehe 10/5/2013 ambayo itakuwa siku ya
siku ya IJumaa na tarehe 3/11/2013 itakuwa siku ya jumapili
Siku
hizi za Alkhamisi Ijumaa na Jumapili ambazo Jua na Mwezi utapatwa zina
athari ya moja kwa moja kwa maisha yetu, Alkhamisi inatawaliwa na
Sayari ya Jupite r ambayo inahusika na Serikali, Wizara. Safari, na Magomvi,
Siku
ya Ijumaa inatawaliwa na Sayari ya Venus au Zuhura ambayo inahusika na
Muafaka, Urafiki,, Mapenzi, Ndoa, Masikilizano, Mapatano, Mambo ya
Muziki, Wasanii, na Michezo.
Siku
ya Jumapili inatawaliwa na Sayari ya Jua ambayo inahusika na Kiburi,
Nguvu, Ufahari, Kuona haya, wanasiasa, madereva, mafundi wa mambo ya
moto na magari.
Huu
Mwaka wenyewe 2013 namba mbili za mwisho 13 ukizijumlisha
unapata 4 ambayo ni nyota yaKaa au Cancer ambayo inahusikana ,Kilimo,
Mapenzi, Unyonge, Kufanya vitu kwa vishindo, Siri na kuvumbuka kwake,
Kuvunjika biashara na kutimia kwa haja, Mvua na Mafuriko na Majanga ya
asili.
KUTOKANA NA HAYO MAELEZO:-
Hali ya Kijamii:
Natabiri:
kwamba katika Mwaka huu wa 2013 Ndoa nyingi zitavunjika. Watu wengi,
wakiwemo Mawaziri na Viongozi Waandamizi wake kwa waume, watajikuta
katika kashfa ya Ngono, Kufumaniwa au kufumania na kupigana kiasi cha
baadhi yao kuuawa.
Natabiri; Kuwa maisha katika mwaka huu yatakuwa mazuri, lakini kwa Watanzania watakaojifunga mikanda kuelekea katikati ya mwaka 2013.
Natabiri: Maradhi
ya watoto kuongezeka katika Mwaka huu wa 2013 na hasa ya kifua na
kichwa. Wanawake wengi wajawazito watapoteza maisha kwa kujifungua na au
kuzaa kwa matatizo makubwa ambayo hayajawahi kuonekana.
Natabiri: Ajali zitakuwa nyingi, kuchafuka kwa bahari kutakuwako kwa wingi na kutakuwa na hofu ya watu wengi kuuawa.
Natabiri: Kutokea
kwa mioto mikubwa kwenye miji mikubwa, Njaa kuongezeka, ukosefu wa
maadili, wafanyakazi kuwapiga mabosi wao, uongo mwingi kwa maana ya
propaganda,
Natabiri: Umbeya utakua kwa kiwango kikubwa mwaka huu wa 2013, pamoja na masengenyo.
Natabiri vifo vya Mashujaa au wale watakojiona ni mashujaa.
Natabiri:
wingu zito la vifo vya ghafla kwa watunzi wa hadithi na vitabu,
Waandishi wa habari, Wanasiasa na Wasanii na muda huu itakuwa mbaya
zaidi ya mwaka jana.
Hali ya Kisiasa:
Natabiri: Viongozi
wengi wakiwemo Wabunge, Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Wenyeviti wa vyama na
Makatibu wao watatoa matamshi ya utatanishi na kusababisha khofu na
mitafaruku mikubwa itakayowafanya watu kupigana.
Hata
hivyo, hali hiyo itadumu kwa muda mfupi. Kwani baadhi ya viongozi
watalazimika kukaa pamoja na kukubaliana mambo baina yao na kurejesha
hali ya utulivu na amani.
Natabiri: Wabunge
wengi katika Bunge la Jamhuiri ya Muungano wa Tanzania wataungana
katika masuala yatakayohusu Utaifa bila kujali itikadi zao za kivyama
au kimajimbo. Hata hivyo, nyota zinaonesdha kuna baadhi ya wabunge
wataanguka Bungeni wakati wa majadiliano.
Kinyota haionekani kuwa kutakuwa na athari lakini itapaswa kufanyika juhudi za ziada kuokoa maisha yao.
Natabiri Rais
Jakaya Kikwete maarufu kama “JK” kufanya mambo ya ajabu na
yasiyotabirika na ataungwa mkono kwa asilimia 100 na wananchi wote wa
Bara na Visiwani.
Natabiri JK atatenda maamuzi magumu katika mwaka 2013 kiasi cha dunia kushangaa.
Natabiri: JK
ataendelea kupata wasaidizi sadifu hasa kwa upande wa Uwaziri. Vile
vile nyota za Mawaziri Harrison Mwakyembe, John Pombe Magufuli na
Khamisi Kagasheki zitazidi kungara Mwaka huu na kuungwa Mkono na
Wananchi
Natabiri JK
ataunganisha nchi na kuwa moja yenye uimara wa Utaifa kuliko
watangulizi wake. na atashirikiana zaidi na Wanasiasa na viongozi wa
dini kuondoa mtikisiko wa uvunjifu wa amani uliokuwapo nchini mwaka
jana.
Natabiri Chama
kimoja cha siasa hapa nchini kuchochea kujitenga na kuunda Taifa lake.
Hata hivyo, kusudio hilo halitafanikiwa. Kwani litapingwa na Watanzania
wote kwa kauli na vitendo.
Natabiri:. Natabiri Tanzania kushinda kwa kishindo kwenye mgogoro wake na Malawi kuhusu Ziwa Nyasa bila kupigana vita.
Hali ya Kibiashara:
Natabiri: Mauzo
ya bidhaa yataongezeka na kuongeza neema na watu kufaidika katika
biashara. Pia mwisho wa mwaka huu wa 2013 mvua zitaongezeka na mazao
yatakuwa mengi.
Natabiri: Wafanyabiashara wengi na hasa wajasiriamali kufanikiwa katika kazi zao.
Natabiri: Neema itawaangukia wajasiriamali wa aina zote hapa nchini kwa mwaka huu.
Natabiri wawekezaji wengi zaidi mwaka huu watajikita kwenye biashara ndogondogo kuliko ilivyokuwa katika miaka iliyopita.
Natabiri: Sakata
la gesi ya Mtwara litatulia na kumalizika kwa amani katika mwaka huu wa
2013 kwa wananchi wote kuungana na kuunga mkono matumizi yake kwa faida
zaidi ya Taifa badala ya jimbo au majimbo
Natabiri: Nchini Kenya ambao ni Majirani zetu Muungano
wa CORD ukiongozwa na Raila Odinga kushinda uchaguzi wa Kenya ambao
utakuwa wa amani na utulivu na kuwashinda Kina uhuru Kenyatta na Ruto na
Muungano wao wa JUBILEE na ule wa Musalia mudavadi unaoitwaAMANI
Maalim Hassan Yahya Hussein
No comments:
Post a Comment