Utamaduni wa Afrika inajumuisha tamaduni zote ambazo ziliwahi kuwa katika bara la Afrika.
Mpasuko mkuu ni kati ya Afrika ya Kaskazini (pamoja na Pembe ya Afrika),] ambayo ni sehemu ya Kiislamu , na Afrika ya Sub-Sahara, ambayo imegawanywa katika idadi kubwa ya tamaduni za kikabila. Mikasama kuu ya kikabila ni Afro-Asiatic (Afrika ya kaskazini, Chad, Pembe ya Afrika), Niger-Congo (sanasana Kibantu) katika sehemu kubwa ya Sub-Sahara ya Afrika , Nilo-Saharan katika maeneo ya Sahara na Sahel na sehemu za Afrika ya Mashariki na Khoisan (wazawa wachache wa Afrika Kusini.Dhana ya utamaduni wa Pan-African ulijadiliwa kwa makini katika miaka ya 1960 na 1970 katika muktadha wa harakati ya Négritude , lakini dhana hii imepoteza mtindo katika masomo ya Afrika. Usambazaji pana wa Kibantu katika Afrika ya Sub-Sahara, unaojumuisha maeneo ya Afrika ya Magharibi, Afrika ya Mashariki, Afrika ya Kati na vilevile Afrika ya Kusini ni matokeo ya upanuzi wa Kibantu wa milenia ya 1 BK. Utumizi pana wa Kiswahili kama lingua franca yaonyesha kwa uzaidi Kibantu kama athari ya tamaduni ya "Pan-African".
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgZ0XyW8_PIJdYVUF4PUPpX2wwDAiuo7mp1HBBYjRkKgi8xasghl1IDv3c9uxn6U_C5T_ge19KSJ2b8DKOKhCTlJ2gy3DKtVzWj-MI79x3i5haHS30T_Z5lyHYkq_4pR6VzZGPkqfrQQcnX/s200/mamangoma.bmp)
TANZANIA
orodha ya makabila ya Tanzania inaweza kuwa na matatizo kwenye majina haa, kwa sababu mbalimbali.
Orodha hii inatokana na orodha ya lugha za Tanzania inayopatikana katika Ethnologue, pamoja na tovuti nyingine.Inawezekana kwamba baadhi ya majina ya makabila ni majina ya lugha au lahaja badala ya makabila, na labda majina mengine yaliandikwa vibaya.
Juu ya hivyo, hakuna ufafanuzi wa wazi kusema kikundi fulani ni kabila au siyo. Vikundi kadhaa katika orodha hii vina wenyeji mamia tu, lakini vikundi vingine vina mamilioni ya watu; labda kila kikundi kinaitwa "kabila," lakini ni jamii za aina tofauti kabisa. Vikundi katika ukurasa huu vimeorodheshwa kuwa vikundi tofauti kutokana na ushahidi kutoka Ethnologue kutofautisha lugha zao.
Hii ni orodha ya makabila ya watu ambao wamekuwa wanaishi tangu zamani katika eneo ambalo sasa linaitwa Tanzania, pamoja na makabila yaliyogawiwa na mipaka baina ya Tanzania na nchi za jirani.
Orodha hii haizingatii makabila yanayoishi katika Tanzania kama wakimbizi tu, hasa kutokana na vita katika nchi za jirani. Vilevile ukurasa huu hauorodheshi vikundi vya wahamiaji kutoka nchi za kigeni, kama wahamiaji au wazao wao kutoka Uarabuni au Uhindi.
- Waalagwa (pia wanaitwa Wasi)
- Waakiek
- Waarusha
- Waassa
- Wabarabaig
- Wabembe
- Wabena
- Wabende
- Wabondei
- Wabungu (au Wawungu)
- Waburunge
- Wachagga
- Wadatoga
- Wadhaiso
- Wadigo
- Wadoe
- Wafipa
- Wagogo
- Wagorowa (pia wanaitwa Wafiome)
- Wagweno
- Waha
- Wahadzabe (pia wanaitwa Watindiga)
- Wahangaza
- Wahaya
- Wahehe
- Waikizu
- Waikoma
- Wairaqw (pia wanaitwa Wambulu)
- Waisanzu
- Wajiji
- Wajita
- Wakabwa
- Wakaguru
- Wakahe
- Wakami
- Wakara (pia wanaitwa Waregi)
- Wakerewe
- Wakimbu
- Wakinga
- Wakisankasa
- Wakisi
- Wakonongo
- Wakuria
- Wakutu
- Wakw'adza
- Wakwavi
- Wakwaya
- Wakwere (pia wanaitwa Wanghwele)
- Wakwifa
- Walambya
- Waluguru
- Waluo
- Wamaasai
- Wamachinga
- Wamagoma
- Wamakonde
- Wamakua (au Wamakhuwa)
- Wamakwe (pia wanaitwa Wamaraba)
- Wamalila
- Wamambwe
- Wamanda
- Wamatengo
- Wamatumbi
- Wamaviha
- Wambugwe
- Wambunga
- Wamosiro
- Wampoto
- Wamwanga
- Wamwera
- Wandali
- Wandamba
- Wandendeule
- Wandengereko
- Wandonde
- Wangasa
- Wangindo
- Wangoni
- Wangulu
- Wangurimi (au Wangoreme)
- Wanilamba (au Wanyiramba)
- Wanindi
- Wanyakyusa
- Wanyambo
- Wanyamwanga
- Wanyamwezi
- Wanyanyembe
- Wanyaturu (pia wanaitwa Warimi)
- Wanyiha
- Wapangwa
- Wapare (pia wanaitwa Wasu)
- Wapimbwe
- Wapogolo
- Warangi (au Walangi)
- Warufiji
- Warungi
- Warungu (au Walungu)
- Warungwa
- Warwa
- Wasafwa
- Wasagara
- Wasandawe
- Wasangu (Tanzania)
- Wasegeju
- Washambaa
- Washubi
- Wasizaki
- Wasuba
- Wasukuma
- Wasumbwa
- Waswahili
- Watemi (pia wanaitwa Wasonjo)
- Watongwe
- Watumbuka
- Wavidunda
- Wavinza
- Wawanda
- Wawanji
- Waware (inaaminika lugha yao imekufa)
- Wayao
- Wazanaki
- Wazaramo
- Wazigula
- Wazinza
- Wazyoba
No comments:
Post a Comment