Ushindi huo uimeifanya timu hiyo kuingia katika
orodha ya timu zilizoshinda mabao mengi katika mashindano ya kimataifa
au ya Bara la Afrika.
Kufuatia matokeo hayo ya mechi ya mchujo ya Kombe
la Dunia, Msumbiji inatakiwa kushinda zaidi ya mabao 10 ili kusonga
mbele, jambo ambalo wengi wanachukulia kama linahitaji miujiza.
Wanawake wa Tanzania wanaingia katika rekodi ya
miongoni mwa timu zilizovuna mabao mengi katika mashindano ya kimataifa
au yale yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).
Timu ya wanawake ya Tanzania ingeongeza mabao
mawili tu ingefikia rekodi iliyowekwa na Pamba ya Mwanza mwaka 1989 kwa
kuwa timu ya kwanza ya Tanzania kushinda mabao mengi katika mashindano
ya kimataifa au yale ya Afrika.
Pamba ya Mwanza iliweka rekodi hiyo baada ya
kuifunga Anse Boileau ya Shelisheli mabao 12-1 katika mechi ya marudiano
ya iliyokuwa michuano ya Kombe la Washindi Afrika iliyochezwa mwaka
1990 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Pia ushindi huo ulikuwa rekodi ya Afrika kwani
hadi kufikia mwaka huo hakuna timu ya bara hilo iliyowahi kushinda kwa
idadi kubwa ya mabao katika mashindano mbalimbali.
Pamba iliitoa Anse Boileau katika mwaka huo kwani
katika mchezo wa kwanza uliochezwa huko Victoria, Shelisheli, timu hiyo
iliibuka na ushindi wa mabao 5-0 na kuifanya kusonga mbele kwa mabao
17-1.
Kwa mujibu wa tovuti ya Televisheni ESPN, rekodi
ya Pamba ilivunjwa mwaka 1994 na Mbilinga ya Gabon, ambayo iliicharaza
Renaissance ya Chad mabao 13-0 katika mechi ya Kombe la Washindi barani
Afrika mwaka 1994.
Pia rekodi za shirikisho la kimataifa
linalojihusisha na historia na rekodi za soka zinaonyesha kuwa rekodi ya
dunia inashikiliwa na Deportivo Arabe Unido ya Panama, iliyowahi
kuichakaza Deportivo Jalapa ya Nicaragua 19-0 katika mechi ya Klabu
Bingwa ya CONCACAF.
Rekodi za shirikisho hilo la kimataifa zinaonyesha
kuwa Ajax Amsterdam ya Uholanzi inashikilia rekodi ya Ulaya baada ya
kuiliza Red Boys Differdange ya Luxembourg katika mechi ya kwanza ya
UEFA mwaka 1984.
Kwa bara la Oceania, timu ya Central United FC ya
New Zealand ndiyo inayoshikilia rekodi baada ya kuilaza Lotoha’pai ya
Tonga mabao 16-0 mwaka 1999.
No comments:
Post a Comment